PSG Yanawa Mikono Kwa Kyllan Mbappe

 

PSG Yanawa Mikono Kwa Kyllan Mbappe
 Kyllan Mbappe

Uongozi wa Klabu Bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain unajipanga kumuuza Mshambuliaji wake Kyllan Mbappe msimu huu ili kuepuka kumwachia akiwa huru baada ya kumaliza mkataba wake msimu ujao.


Raia huyo wa Ufaransa mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao (2023/24), ambapo una kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja.


Usajili unatarajiwa kufungwa Julai 31, mwaka huu ambapo tayari Mbappe ameshaandika barua kwa uongozi kwamba hataongeza mkataba mpya, japokuwa na kulikuwa mazungumzo kwa miezi kadhaa ambayo hawakufikia muafaka.


Ishu ya Nabi bado kizungumkuti Young Africans

Taarifa iliyotoka katika mtandao wa klabu hiyo imeeleza wanatarajia kumuuza Mbappe kabla ya kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu ujao, ili kuepuka mchezaji huyo kuondoka akiwa huru.


Hata hivyo uongozi huo umesema unatarajia kumuuza mchezaji huyo kutokana na baadhi ya timu kubwa Ulaya kuonyesha nia ya kuihitaji saini yake.


Real Madrid ni moja ya timu ambazo zilishaanza kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo kwa muda mrefu bila mafanikio.


Mbappe ambaye alijiunga na PSG kwa mkopo mwaka 2017 akitokea Monaco, kabla ya kusajiliwa kwa mkataba wa muda mrefu wa euro milioni 180, tayari ameshafunga mabao 212 na katika mechi 260 alizocheza.


Ratiba EPL kuanikwa wazi Julai 15

Kwa upande wa timu yake ya taifa ya Ufaransa, amefunga mabao 38 katika mechi 68 ikiwemo hat-trick’ ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar msimu uliopita wakati Ufaransa ikitolewa na Argentina kwa mikwaju ya penalti.


Mbappe alimaliza msimu huu akiwa mfungaji bora kwa mara ya tano katika misimu sita huku akiisaidia timu kupata ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa mara tano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.